Ngoma zetu
Kama ilivyo kwa jadi zote. Wanyisanzu wana ngoma ambazo huchezwa katika matukio mbalimbali ya kijamii kama harusi n.k. Ngoma kuu inajulikana kama "Nki'ninta" hii huchezwa na wanaume na wanawake rika zote. Hujipanga mistari miwili wakitizamana na wanaume huruka kwa mirindimo maalumu wanawake hutingisha mabega.
Njuga au Nkinda kwa kinyisanzu hutumika kwa kuvaliwa miguuni nazo hutoa milio pia. pia kuna mbutu ambazo hutumika zaidi kwa shughuli za dini za asili yaani wapagani. Mbutu ni bomba kama pembe ndefu ambazo hupulizwa na kutoa mlio. Wapiga mbutu waliweza kutambulika kwa kuwa midomo yao ilibadilika rangi na kuwa pink. Nitawaletea habari zaidi. (Kwa hisani ya simulizi ya ndugu na jamaa)