Friday, June 8, 2012

KIPEYO

Kipeyo au Lukulu(Kinyisanzu) ni chombo cha kunywea vinywaji mbali mbali kwa kabila la wanyisanzu. Wenyeji huweka maji ya kunywa kwenye mitungi ya udongo wa mfinyanzi ambapo huwa ya baridi na kuwa na ladha na harufu nzuri.

Kinywaji pendwa ni togwa ya unga wa mtama hujulikana kama magai. Watafiti waligundua kuwa ni kinywaji chenye lishe na viambata vinavyozuia magonjwa ya kuhara kwa watoto. Kwa sasa utaweza kuona kinywaji hiki kitamu kisicho na kilevi kikiuzwa hata Singida mjini. Kinywaji hiki kimepata umaarufu na makabila mbali mbali. Ni utamaduni wa wanyisanzu kumkarimu mgeni kwa magai na karanga ziwe mbichi au za kukaanga.

3 comments:

  1. Hakika MAGAE ni kinywaji chenye lishe bora, na pia HESHIMA KUBWA kwa mgeni. Pia huashiria ukarimu, ambayo ni asili ya Mwafrika na Mnyisanzu kwa ujumla. Nashukuru sana kwa Blog hii kuwa hewani, tunapata nafasi ya kuchangia mada mbalimbali, kuelimishana, n.k.
    Big up sana Dr Grace na Zenna kwa juhudi kubwa mnazofanya. Tuko pamoja.

    ReplyDelete
  2. Dah! umenikumbusha nyumbani Nkinto tulivyokuwa tunakimbizana kule "kunkhaha na kung'wadeluh"

    ReplyDelete
  3. Ngoma ya Kinyisanzu ya Nkininta siku hizi siisikii. Jamani, kama kuna mtu anapenda tujiunge, tuanzishe kikundi cha ngoma za kinyisanzu hapa dar es Salaa. Tudumishe desturi zetu. Kikundi hiki kinaweza pia kukodishwa wakati wa sherehe mbalimbali kama harusi, n.k. mtu ambaye yuko tayari naomba tuwasiliane kwa 0713 520106 au 0754 264906. Watoto wetu watapoteza kabisa uasilia wetu kama tusipokuwa makini, hasa walioko mijini. Wengi wana mix nyimbo za Kinyiramba na za Kinyisanzu.
    Ukisema "Saulaa ee, Saula kele ketunga ee Saula" utawaona wanavyokukodolea macho!!!! Sio makosa yao, ni ya kwetu.

    ReplyDelete