Thursday, June 28, 2012

Vyakula vikuu vya Wanyisanzu
Vyakula vya asili vya Wanyisanzu ni ugali wa mtama ukiambatana na mboga ya mlenda wa kusaga(Ndalu) au fresh, au mboga mbali mbali za kijani zilizokaushwa kama nsansa, nsonga, kwa kawaida nyama hukaushwa na kuwekwa chumvi ikijulikana kama "mintanda" Vyakula hivi husindikizwa na maziwa ya mtindi. 

Kwa upande wa matunda, kabila hili lilitegemea zaidi matunda ambayo si kutoka bustanini ila matunda yaliojiotea yenyewe kama matogo, mbura,furu, nsalati, nkuyu, ngumo, ntundwa, lade, matini n.k. Wenyeji pia hupendelea kunywa togwa ya unga wa mtama na pombe za kienyeji.

Hapo zamani hakukuwa na mashine za kusaga nafaka, mawe yalichongwa na kuitwa Lwala (jiwe kubwa) na dogo (Nsio) hivi vinatumika kusaga nafaka. kwa baadhi ya maeneo bado hutumia haya mawe kusaga nafaka. Nitaendelea kuelezea zaidi na kuweka taswira nitakapotembelea huko na kupewa habari zaidi.  (chanzo ni simulizi toka kwa ndungu mbali mbali). Asante Aunt Frida Mzengi na Uncle Paulo Mtiko kwa michango yenu.
                                                              Mlenda wa kusaga (Ndalu).

1 comment:

  1. Yani natamani kusonga ugali wa dona sasa hivi, nile hizi ndalu. Duh!!!!

    ReplyDelete