Sunday, October 7, 2012

Utamaduni wa kazi za mikono (Hand craft art)






Kazi za mikono ambazo zimekuwa zikifanywa na wanyisanzu kwa miaka mingi ni ushonaji wa trays au vikapu vinavyojulikana kama "Vitotoo" vikiwa vidogo au Visonzo vikiwa vikubwa. Hivi hushonwa kwa nyasi za asili na sindano maalumu. Huongezwa nakshi za rangi za mikeka na maua mbali mbali. Miaka ya nyuma walitengeneza maumbo ya mduara zaidi, kadri siku zinavyobadilika wamekuwa wakibuni mitndo mbalimbali kama ilivyo hulka ya mitindo kubadilika ili kuendana na wakati.



Zaidi ya urembo, vitu hivi vina matumizi kama vile hutumika makanisani kuwekea sadaka na zaka, unaweza kuweka matunda mezani, maua, kama table mats n.k. inategemea na mtumiaji. Kwa miaka ya sasa mapambo haya yameenea nchi nzima.

No comments:

Post a Comment