Thursday, October 11, 2012

NDOA ZETU

Kama ilivyo katika mila za mataifa na makabila yote. Nitaongelea kuhusu mila ya ndoa za wanyisanzu. Kwa vile sijapata muda wa kuwapata wazee wenyewe wanielezee zile za asili zilikuwaje. Natarajia wadau wangu wanaoelewa watanisaidia kwenye maoni. Kwa miaka ya sasa haiangalii sana unaolewa na mtu anayetoka kabila au ukoo gani. 

Kwa simulizi toka kwa mama yangu. Zamani ilikuwa kijana akimpenda msichana, basi alitoa taarifa. Huyo binti alifuatiliwa ukoo wake kwa karibu kuangalia kama ukoo ule wana tabia gani, je wana magonjwa ya kurithi n.k. Endapo atakubalika basi alitafutwa mshenga wa kwenda kwa familia ya msichana. Huko walipangiwa jinsi ya familia hizi watakavyokuja na waje vipi na nini. Mahari (kinyanzala) ilipangwa kama ni ngombe wangapi na mazao kiasi gani.

Baada ya kufuata taratibu hizi, baada ya kuingia dini, ndoa ilifungwa kanisani kwa wakristo. Sitaongelea dini zingine na wapagani kwani sina taarifa sana. Kumbukumbu zangu za utotoni, nilishuhudia maharusi wakitupiwa maua toka kanisani wakitembea kwa miguu na kuimbiwa nyimbo za kuwasifu n.k. 

Watu walikuwa wakarimu, hakukuwa na kadi za mualiko wala meza kuu. Nyumbani kuliandaliwa makande ya mtama(mpeke). Kinywaji kilikuwa togwa ya mtama na pombe. Ng'ombe alichinjwa na nyama kuliwa. Ngoma zilichezwa na wana kijiji walifurahi.

4 comments:

  1. kwa muda huo ilikuwa pouwa sana ila kwa sasa mambo yamebadilika sana!but ilikuwa njia nzuri sana ya kupata mke au mume,kwa ushauri wangu mimi naona ni vyema kukopi mambo yote yale ya zamani ambayo ni yamsingi yatatusaidia katika maisha yetu ya sasa.

    ReplyDelete
  2. Ndiyo Hewizet, siku hizi mambo mengi kabla ya Harusi. Kitchen party, send off. Bag party.Hatujiulizi je vinasaidia nini? Au ndiyo vinaleta furaha? Michango mingi, ambayo tungeweza kuwekeza kwenye elimu. Ni watoto wangapi wako majumbani kwa vile wameshindwa kulipa ada vyuoni? Je hii michango ingefanyiwa harusi kwa gharama ya chini na baki ikachangia elimu. Ni vigumu kuwa shawishi watu wabadilike. Ila iko siku wataelewa.

    ReplyDelete
  3. Kuna jambo moja nahitaji kufahamu; umegusia swala zima la mahari (kinyanzala) ni kitu gani kinatolewa kuwa ndiyo mahari. Na kinatolewa kwa mode ipi. Na ni nani anapanga kitolewe kitu flani na ni vigezo vipi vinatumika kujua kiasi anachopaswa kulipa mtu. Ukienda kwa wenzetu wasukuma kama mdada ni mweupe ujue hapo zitakutka ng'ombe nyingi mno

    ReplyDelete
  4. Kwenye mahari kuna vitu vinavyotolewa na vina majina kama Mkaja wa Bibi n.k. Ninavyojua kuna mbuzi/ng'ombe, blanket na pesa kwa siku hizi. Ningependa sana kuja na habari za kimila endapo nitaenda kijijini. Shangazi yangu Mama W. Msindai aliyekuwa ananihadithia na kuandika historia yetu bahati mbaya alifariki. Nafuatilia sana nipate writings zake ili niziweke humu. Alitaka atoe kitabu ila haikuwa hivyo. Nitajitahidi kupata hizi habari hata kwa wachangiaji wanaofahamu.

    ReplyDelete